HUDUMA ZA MANA

Lengo kuu la Huduma hii ni kueneza Injili ya Yesu Kristo kwa watu wote.

Fahamu zaidi...
 
 


    Vipindi vya Redio

Ili kulileta Neno la Mungu karibu na wewe zaidi, Huduma ya Mana inaandaa na kurusha baadhi ya mafundisho ya Neno la Mungu kwa njia ya redio kadhaa hapa nchini Tanzania.

Ili kufahamu zaidi redio hizo na siku na saa ya vipindi vyetu, bonyeza hapa.

   

BARUA YA MWEZI APRIL 2013.

        Na tena, ikiwa msichana umempata “Ibrahimu wako” na ukaolewa naye kwa msaada wa Mungu, usishangae ukikuta tumbo lako la uzazi likipata vita na unashindwa kuzaa!

       Naamini unaweza ukaelewa kwa nini Sara alipata shida ya kuzaa kwa Ibrahimu wake; na kwa nini Rebeka alipata shida ya kuzaa kwa Isaka wake; na kwa nini Raheli alipata shida ya kuzaa kwa Yakobo wake; na kwa nini Hana alipata shida ya kuzaa kwa Elkana wake!

       Ni ili wasiweze kupitisha wazaliwa wa kwanza wa haki ili Mungu apate kuwatumia kama lango katika kizazi kilichokuwa kinafuata baada yao. Fuatilia mwenyewe kwenye biblia ulione hili!

       Utaona ya kuwa Sara alimzaa Isaka, Rebeka alimzaa Yakobo, Raheli alimzaa Yusufu, na Hana alimzaa Samweli!

        Pia – utaelewa baada ya kukueleza hayo, Ibrahimu alipata mzigo mkubwa moyoni wa kuona ya kuwa mtoto wake Isaka anapata msaada wa Mungu katika kuoa kwake.

        Ibrahimu alimweleza mfanyakazi wake aliyemtuma kumtafutia Isaka mke ya kuwa

“Bwana, Mungu wa mbingu aliyenitoa katika nyumba ya babaangu,… yeye atampeleka malaika wake mbele yako” (Mwanzo 24:7).

        Unadhani Ibrahimu alilijuaje hili, la kuwa Mungu wake amemtuma malaika wake kwa kazi maalumu ya kuhakikisha ya kuwa – Isaka aliyekuwa mzaliwa wake wa kwanza kwa haki anapata mke sahihi? Ni lazima Ibrahimu alikuwa anaomba juu ya kuoa kwa Isaka kwa mzigo sana, huku akijua umuhimu wa Isaka kama lango na kwa hiyo Mungu hataruhusu aoe mwanamke yeyote tu!

         Shetani aliwapiga vita sana wazaliwa wa kwanza juu ya hili kiasi kwamba anawafanya wazae watoto wao wa kwanza nje ya ndoa!

         Una mzigo wa kiasi gani moyoni mwako wa kumuombea mzaliwa wako wa kwanza – wa kiume juu ya kuoa kwake au wa kike juu ya kuolewa kwake?

         Ndiyo maana nakushauri Mungu akupe kuona umuhimu huo, na pia akupe nguvu za kumwombea ipasavyo juu ya maamuzi ya kuoa au kuolewa kwake, na/au juu ya ndoa yake!

Tuzidi kuombeana.

Christopher na Diana Mwakasege.

  <<<Nyuma

 
Mitandao ya Kijamii
 
 
     

 

 

 

 

 

 

     
 

Ibariki Israeli Pamoja Nasi

Habari za Huduma

Mafundisho ya neno la Mungu

 
Sasa unaweza kutembelea taifa la Israeli kwa mafunzo ya kiroho pamoja nasi mara nne kwa mwaka. Kufahamu zaidi kuhusu huduma ya Israeli,
Bonyeza Hapa.
Karibu ufuatilie habari ,matukio na mabadiliko mbalimbali  yanayohusu huduma ya MANA pamoja na watendajikazi katika huduma.
Bonyeza Hapa kwa maelezo zaidi
Karibu ujisomee mafundisho ya Neno la Mungu katika tovuti hii sasa.
Bonyeza hapa
 
 
|Home|  |Kuhusu MANA |    |Nunua|      |Mafundisho|     |Maombi|     |Ratiba|   |Shuhuda|   |Barua Za Mwezi|   |Israel|

Haki zote zimehifadhiwa © Huduma Ya MANA TANZANIA.