|
|
| ||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Salamu katika Jina la Yesu Kristo. “Kwa sala zote na maombi mkisali kila wakati katika Roho, mkikesha kwa jambo hilo na kudumu katika kuwaombea watakatifu wote” (Waefeso 6:18) Maneno haya “ kwa sala zote na maombi” katika tafsiri nyingine yana maana hii: “Kwa aina zote za sala na maombi.” Hii ina maana kuna aina za maombi na sala zaidi ya moja. Na Biblia inaweka wazi ya kuwa tunahitaji kujua aina zote za sala na maombi. Kujua aina zote za sala na maombi ni mojawapo ya silaha za mkristo dhidi ya shetani. Kwa maana imeandikiwa; “ Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shetani. Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu….” (Waefeso 6:11-13) Baadas ya Mtume Paulo kuandika hayo maneno akaanza kuorodhesha aina mbali mbali za silaha kama vile ‘kweli viunoni’; ‘dirii ya haki kifuani’; ‘Utayari miguuni’; ‘Ngao ya imani’; ‘Chapeo ya wokovu’; ‘Upanga wa Roho ambao ni neno la Mungu’ – halafu akaiweka pia ‘sala zote na maombi’ kama silaha mojawapo ya mkristo dhidi ya mashindano yake na shetani. Biblia inaposema “Vaeni silaha zote za Mungu” ina maana ni silaha ambazo Mungu anampa mtu; na siyo mtu mwenyewe anayejitafutia hizo silaha. Kwa hiyo ikiwa maombi ni silaha ina maana ni maombi ambayo chanzo chake ni Mungu, na Mungu anampa mtu maombi hayo ili aombe. Na maombi hayo Mungu atayatumia kumpiga nayo shetani akimsaidia mtu anayeomba na anayeombewa. Ni muhimu ujue ya kuwa mahali popote palipo na silaha pana upinzani au panatarajia upinzani ambao kuzimwa kwake ni kwa kutumia silaha za aina hiyo iliyoandaliwa. Maandiko yanatuamiba ya kuwa kwa sababu kuna vita,basi tumepewa silaha za kutusaidia kupigana na kushinda. Si maombi yote ambayo ni silaha Lakini si maombi yote ambayo ni silaha ya kutusaidia kupambana na shetani. Tukitafsiri ya kuwa maombi ni mazungumzo kati ya mwanadamu na Mungu wake, basi tunafahamu ya kuwa si mazungumzo yote yanayofanyika katika maombi yanahusisha ugomvi wa mwombaji na shetani. Wakati mwingine mtu anapoingia katika maombi, anazungumza na Mungu mambo yanayohusu wao wawili. Kwa mfano anaweza kuwa ameamua kuomba ‘maombi’ ya kushukuru yasiyohusisha vita yoyote. Tatizo lililopo kwa watu wengi ni kwamba wanajua aina moja tu au aina chache sana za maombi. Kujua aina moja tu au aina chache za maombi kumefanya wengi washindwe katika mshindano waliyonayo na shetani. Kuomba maombi ambayo si silaha yanafanya shetani asiachie kile unachotaka aachie. Zipo aina mbalimbali za maombi, na pia zipo aina mbalimbali za kuomba. Taratibu zake zinatofautiana pia. Ili uweze kuomba vizuri na kwa mafanikio kuna mambo ya msingi ambayo unahitaji kujua. Kwa mfano hebu soma tena maneno haya ya Waefeso 6:11-13: “Vaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kuzipinga hila za shetani.” Kwa hiyo lengo la Mungu la kutaka tuvae silaha zake zote ni ili tupate “Kuweza kuzipinga hila za shetani”; ambayo ina maana tusipovaa silaha zote za Mungu, hila za shetani zinaweza kutushinda. “Kwa sababu kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho. Kwa sababu hiyo twaeni silaha zote za Mungu, mpate kuweza kushindana siku ya uovu….” Sasa, unapoendelea kusoma waraka huu aliouandika Mtume Paulo kwa Waefeso utaona ya kuwa maombi yanayozungumzwa hapa ni sehemu ya silaha ambazo mkristo amepewa ili aweze kushindana na shetani na kushinda. Lakini ni vizuri ujue ya kuwa huwezi kushindana vizuri na kushinda kama hujui kwa nini unashindana na mnashindania kitu gani na shetani. Tunashindana na shetani juu ya nini? Mungu alipomuumba mwanadamu alikusudia ya kuwa awe ndiye mungu wa dunia hii kwa hiyo akaviweka vitu vyote chini yake ili avitawale (Mwanzo 1:26-28; Zaburi 8:4-8). Kwa lugha iliyo nyepesi ni kwamba Mungu alitaka au aliamua mwanadamu ndiye awe mungu wa dunia hii na vyote vilivyomo viwe chini ya uongozi wake. Ndiyo maana imeandikwa hivi; “Mimi nimesema, Ndinyi miungu, na wana wa Aliye juu nyote pia” (Zaburi 82:6) Mungu anawaita wanadamu aliowaumba miungu. Tunaona jambo hili likisisitizwa na Yesu wakati alipokuwa akijibu tuhuma dhidi yake ya kuwa amekufuru kwa kujifanya yuko sawa na Mungu. Yesu naye akajibu tuhuma hizi kwa kusema: “ Je! Haikuandikwa katika torati yenu ya kwamba, Mimi nimesema, Ndinyi miungu? Ikiwa aliwaita miungu wale waliojiliwa na neno la Mungu; (na maandiko hayawezi kutanguka); je! Yeye ambaye Baba alimtakasa, akamtuma ulimwenguni, ninyi mnamwambia, unakufuru; kwa sababu nalisema, Mimi ni Mwana wa Mungu?” (Yohana 10:34-36). Ikiwa mwanadamu ndiye aliyekusudiwa na Mungu awe mungu wa dunia hii na kutawala yote, kitu gani kilitokea hadi mwanadamu akaipoteza nafasi na hadhi hiyo na kumwachia shetani? Nasema na kuuliza hivi kwa sababu katika 2 Wakorintho 4:3,4 shetani ameitwa “mungu wa dunia hii” Pia, tunaona ya kuwa Yesu hakubisha wakati shetani anamjaribu na kusema ya kuwa vyote vya ulimwengu amepewa yeye. Tunasoma habari hii ya kwamba:
“(Ibilisi) akampandisha (Yesu) juu, akamwonyesha milki zote za
ulimwengu Pamoja na kwamba Yesu hakumsujudia shetani kama alivyotakiwa, lakini pia hakubisha juu ya usemi wa kuwa vitu vyote vya ulimwengu vimo mikononi mwa shetani. Wasomaji wa biblia wanajua ya kuwa Yesu ndiye aliyehusika na uumbaji wa vitu vyote kufuatana na Yohana 1:1-3,14. Kwa hiyo anajua ya kuwa ulimwengu na vyote vilivyomo alikabidhiwa Adamu na wazao wake na si shetani. Ikiwa Mungu hakumpa shetani dunia hii, ni nani basi alimpa isipokuwa mwanadamu mwenyewe! Adamu alipoumbwa alipewa ulimwengu na vyote vilivyomo kuwa urithi wake na ya kwamba avitawale yeye pamoja na uzao wake. Lakini aliporuhusu dhambi ingie mashani mwake, si tu kwamba alimkosea Mungu, lakini pia alipoteza urithi huo aliokabidhiwa na kumpa shetani urithi huo wa ulimwengu. Ndiyo maana shetani akaitwa mungu wa dunia hii na mmiliki wa yote yaliyomo (2 Wakorintho 4:3,4; Luka 4:5,6). Dhambi ilimpa shetani kuwa mungu wa dunia hii, na wakati huo huo mwanadamu akapoteza uhalali, mamlaka na nguvu za kutawala ulimwengu huu. Na tangu wakati huo mwanadamu na vitu vyote ulimwenguni vikawa chini ya shetani. Kazi mojawapo ya msalaba Lengo la Mungu kumkomboa mwanadamu ni kurudisha uhusiano naye na kumpa uzima wa milele ambao unampa nafasi ya kupokea upya sura ya Mungu aliyoipoteza. Lakini pamoja na lengo hilo zuri, katika kumkomboa mwanadamu alitaka pia amrudishie mwanadamu urithi wa ulimwengu na vyote vilivyomo. Ndiyo maana Yesu Kristo alipokuja pale msalabani alitulipia mshahara wa dhambi yaani mauti na akatupa nafasi ya kupokea tena uzima wa milele kwa njia ya Yeye (Warumi 6:23). Lakini pamoja na jambo hili pale msalabani Yesu alitukomboa toka kwenye laana ya torati; “ Ili kwamba baraka ya Ibrahimu iwafikilie Mataifa katika Yesu Kristo, tupate kupokea ahadi ya Roho kwa njia ya imani” (Wagalatia 3:13,14). Kati ya ‘baraka ya Ibrahimu’ inayotakiwa itufikie ni urithi wa ulimwengu na vyote vilivyomo. “Kwa maana ahadi ile ya kwamba atakuwa mrithi wa ulimwengu alipewa Ibrahimu na uzao wake, si kwa sheria bali kwa hakialiyohsesabiwa kwa imani. Maana ikwa wale wa sheria ndio warithi, imani imekuwa bure, na ahadi imebatilika. Kwa hiyo ilitoka katika imani,iwe kwa njia ya neema, ili kwamba ile ahadi iwe imara kwa wazao wote; si kwa wale wa torati tu, ila na kwa wale wa imani ya Ibrahimu aliye baba yetu sisi sote” (Warumi 4:13,14,16). Kwa kifupi ni kwamba tunapookoka tunakuwa ‘uzao wa Ibrahimu’ (Wagalatia 3:29), na warithi sawasawa na ahadi. Ahadi mojawapo aliyoahidiwa Ibrahimu na uzao wake (ambao ni pamoja na sisi) ni urithi wa ulimwengu.Ndiyo maana tunasoma katika Warumi 5:17 ya kuwa:
“Kwa maana ikiwa kwa kukosa mtu mmoja mauti ilitawala kwa sababu ya
yule Kwa tafsiri nyingine ni kwamba katika Kristo Yesu tunarudishiwa tena uhalali,mamlaka na nguvu ya kurithi na kutawala ulimwengu na vyote vilivyomo. Muda wa shetani haujaisha Je! Unafahamu ya kuwa Ibrahimu alipewa urithi wa ulimwengu huu wakati shetani bado ni mungu wa dunia hii? Je! Unafahamu ya kuwa sisi tulio uzao wa Ibrahimu kwa imani ndani yake Kristo tumerithishwa ulimwengu huu wakati shetani bado ni mungu wa dunia hii? Je!unajua ni kwa nini Yesu alimpomshinda shetani pale msalabani kwa ajili yetu hakumwondoa kabisa humu ulimwenguni? Na kwa sababu hiyo shetani amekuwa mpinzani mkuu wa mapenzi ya Mungu kutimizwa hapa duniani. Kwa hiyo shetani amekuwa akishandana na wana wa Mungu waliopo hapa duniani ili mapenzi ya Mungu yasitimizwe kwao au kwa ulimwengu. Sababu kubwa inayompa nafasi shetani kufanya upinzani huu ni kwa sababu muda wake aliopewa kutawala ulimwengu huu haujaisha. Ndiyo maana Mtume Paulo alipokuwa anawaandikia Wakorintho ya kuwa shetani ni mungu wa dunia hii, aliandika baada ya Yesu kumaliza kazi yake pale msalabani na kupaa mbinguni. Sasa unaweza ukaelewa kwa nini mapepo yaliwahi kumpigia kelele Bwana Yesu alipokuwa hapa duniani na kusema;
“Tuna nini nawe, Mwana wa Mungu? ‘Kabla ya muhula wetu’ maana yake ‘ kabla ya muda wetu tuliopangiwa kutawala kabla ya kuteswa’. Inaonyesha wazi kabisa ya kuwa mapepo hayo yalikuwa yanaelewa ‘mkataba’ waliongia Adamu na Shetani ya kuwa ulikuwa wa kipindi Fulani, na ya kwamba kikiisha yatateswa. Huu ukweli ndio ulioumpa ujasiri shetani wa kumwambia Bwana Yesu juu ya ulimwengu ya kuwa, “enzi hii yote, na fahari yake, kwa kuwa imo mikononi mwangu, nami humpa ye yote kama nipendavyo” (Luka 4:6). Shetani alijua Yesu anajua sheria, na ya kwamba hawezi akamnyang’anya ulimwengu bila mzao wa Adamu kusema neno la kuhitaji msaada wa kuuingilia mkataba huo. Hii ndiyo sababu kubwa ya maombi ambayo ni silaha; kwa kuwa ni maombi ambayo yanampa Mungu nafasi ya kumsaidia mwanadamu apate kilicho mapenzi ya Mungu au kilicho halali yake ndani ya Kristo ambacho shetani ‘anashindania’ asikipate. Ndiyo maana Mungu huwa anatafuta mtu Kwa nini Mungu anataka tuombe juu ya vitu ambavyo anajua tunahaja navyo?Si atupe tu? Ni kitu gani kinamzuia asifanye hivyo? Kinachomzuia ni hiki. Mtu ni nafsi huru. Mungu alimpa dunia hii aitawale pamoja na vyote vilivyomo.Lakini kwa kutenda dhambi, shetani alichukua nafasi hiyo ya kutawala. Kwa hiyo hadi hapo ‘muhula wa shetani’ utakapokwisha Mungu akitaka kufanya mapenzi yake hapa duniani inabidi apate mtu ambaye atamfahamisha kwanza mapenzi yake ili mtu huyo aombe ndipo Mungu ashuke kuyafanya. Hili ni jambo la ajabu sana. Shetani alibaki duniani akitawala baada ya kushindwa pale msalabani hadi ‘muda wake utakapokwisha’! Kwa hiyo wale wanaotaka ufalme wa Mungu wakati huu na ya kwamba mapenzi ya Mungu yatimizwe ni lazima waombe – kwa ajili yao au/na kwa ajili ya wengine. Ndiyo maana wanafunzi walipoomba Yesu awafundishe kusali aliwaambia waombe hivi;
“Baba yetu uliye mbinguni Jina lako litukuzwe, Ufalme wako Mungu amekuwa akitafuta mtu wa kumfundisha siri hii ili aweze kufanya kazi pamoja naye hapa duniani ili kwa njia ya maombi ufalme wa Mungu ujengwe na mapenzi ya Mungu yatimizwe hapa duniani kama yanavyotimizwa huko mbinguni wakati huu. Tuzidi kuombeana. Ni sisi katika utumishi wa Kristo, Christopher na Diana Mwakasege |
|