|
|
| ||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Salamu katika Jina la Yesu, Mwezi uliopita tulikuletea sehemu ya kwanza ya mafundisho haya ambamo tunakupa “Amri 10 za kukusaidia kufanya maamuzi mazuri katika maisha yako”. Kama tulivyokwishatangulia kukueleza ya kuwa maisha ya mtu ni matunda ya mtiririko wa maamuzi ya mtu binafsi, lakini yanaweza pia yakawa yamechanganyika na maamuzi ya watu wengine yaliyogusa maisha yake. Kwa mfano, unaposoma makala hii katika gazeti hili leo, ni matokeo ya maamuzi ya watu wengi sana, ikiwa ni pamoja na wewe kuamua kuisoma. Kuna maamuzi ya sisi tuliyoiandika. Kuna maamuzi ya wale waliochapa katika ngazi mbalimbali, kuna maamuzi ya wale waliohariri toleo la gazeti hili, kuna maamuzi ya kulinunua – nakadhalika. Katika sehemu ya kwanza ya somo hili tuliyoitoa wiki iliyopita, tulikufundisha juu ya amri 4 kati ya 10 tunazotaka uzijue za kukusaidia kufanya maamuzi mazuri katika maisha yako. Kwa muhtasari tu amri hizo zinasema hivi: Amri ya 1: Usijisumbue wala kuhangaika katika kufanya uamuzi wowote! Amri ya 2: Acha amani ya Kristo iamue ndani yako juu ya jambo, halafu wewe fuata kile ambacho amani ya Kristo imeamua juu ya jambo hilo! Amri ya 3: Usinie makuu kupita imani uliyonayo maana maamuzi yako na utekelezaji wake vinategemea aina na kiwango cha imani uliyonayo! Amri ya 4: Usifanye maamuzi kwa mazoea tu, bali jifunze kumtegemea Roho Mtakatifu! Wiki hii tunataka tuendelee kukuletea mfulululizo huu kwa kukuelezea amri zaidi zifuatazo za kukusaidia kufanya maamuzi: Amri ya 5
Uamuzi ni mbegu.
Kwa hiyo usifanye uamuzi ambao Uamuzi wowote ulionao ni mbegu na uko ndani ya moyo wako. Lakini ukiamua kuusema au kuutekeleza, unaupanda katika maisha yako na katika jamii. Kwa mfano Wagalatia 6:7-9 inasema hivi: “ Msidanganyike, Mungu hadhihakiwi, kwa kuwa cho chote apandacho mtu, ndicho atakachovuna. Maana yeye apandaye …. atavuna …. Tena tusichoke katika kutenda mema; maana tutavuna kwa wakati wake, tusipozimia roho”. Matendo ya mtu ni matokeo ya maamuzi yake – akiyatekeleza atavuna. Uamuzi ni mbegu ambayo unaweza ukaipanda kwa kuitekeleza. Mfano mwingine ni Mithali 13:2: “Mtu atakula mema kwa matunda ya kinywa chake” Uamuzi ni mbegu moyoni mwako lakini unapousema unaipanda hiyo mbegu – na utavuna – usipoyafuta hayo maneno kwa damu ya Yesu ikiwa si maneno mazuri. Kwa hiyo tunakushauri ya kwamba usiseme wala kutekeleza uamuzi ambao hutakuwa tayari kupokea na kufurahia matokeo (au mavuno) yake. Tafakari maneno haya ya Mithali 6:12,14,15 yanayosema hivi: “Mtu asiyefaa kitu, mtu wa uovu; huenda njiani mwenye kinywa cha upotofu. Mna upotofu moyoni mwake, hutunga uovu daima, hupanda mbegu za magomvi. Basi msiba utampata kwa ghafula; ghafula atavunjika, bila njia ya kupona.” Huyu mtu angejua ya kuwa ‘mbegu’ anayopanda toka ‘moyoni’ mwake itazaa ‘magomvi’ yatakayomletea ‘msiba’ labda angebadili maamuzi yake! Amri ya 6
Hesabu gharama
kwanza za uamuzi wako uone kama Yesu mwenyewe alisema katika kitabu cha Luka 14:28 – 30 ya kwamba: “Maana ni nani katika ninyi, kama akitaka kujenga mnara, asiyeketi kwanza na kuhesabu gharama, kwamba anavyo vya kuumalizia? Asije akashindwa kuumalizia baada ya kuupiga msingi, watu wote waonao wakaanza kumdhihaki, wakisema, mtu huyu alianza kujenga, akawa hana nguvu za kumalizia”. Yesu alitaka tuwe waangalifu tunapofanya maamuzi na kuanza kutekeleza maamuzi hayo tusifanye hivyo bila kuhesabu gharama zake. Kwa mfano: Unaweza kuamua kuoa au kuolewa – je! Umehesabu gharama za kudumu ndani ya ndoa hiyo hadi kifo kiwatenganishe? Unapoamua kumtumikia Mungu – Je! Umehesabu gharama za utumishi huo katika mazingira utakayowekwa kutumika? Au utajikuta unasema kama Wana wa Israeli wakati mmoja waliposema “ Kumtumikia Mungu hakuna faida”! (Malaki 3:14). Umeamua kumfuata Yesu katika maisha yako? Je ulikaa chini na kuhesabu gharama zake kabla ya kuutekeleza ili ujue kama unaweza kuendelea kumfuata siku zote za maisha yako? Yesu alisema katika Luka 9:23 ya kwamba:
“Mtu yeyote
akitaka kumfuata, Unapohesabu gharama kwanza kabla ya kutekeleza uamuzi ulionao, kunakusaidia kujipanga vizuri namna ya ‘kuugharamia’! Amri ya 7
Usimshirikishe
kila mtu uamuzi ulionao kwa mategemeo ya kwamba mtu Hii ni kwa sababu si kila mtu atakubaliana na maamuzi yako mengine! Kwa wale waliookoka wanaelewa ya kuwa ikiwa wangewashirikisha watu wote wanaowajua juu ya maamuzi yao ya kuokoka kabla hawajaokoka – kuna wengi ambao wangepinga maamuzi hayo. Yesu mwenyewe alipigwa na Mtume Petro alipoamua kuwashirikisha wanafunzi wake juu ya uamuzi wake wa kwenda Yerusalemu na kufa msalabani. Soma habari katika kitabu cha Mathayo 16:21 – 23. Hebu fikiria kungetokea nini kwa ulimwengu kama Yesu angeamua akubaliane na Mtume Petro na aache kufa msalabani? Maana yake wokovu usingekuwepo kwa jinsi tunavyoujua sasa kwa jinsi tulivyoupata kupitia uamuzi wa Yesu wa kufa msalabani kwa ajili ya wanadamu. Kuna wengine watakutia moyo kama wanakubaliana na ulichoamua – lakini kuna wengine ambao hawatakutia moyo. Kwa hiyo uwe mwangalifu unamshirikisha nani na kwa wakati gani juu ya maamuzi yako mbalimbali. Ikiwa unatafuta kuuthibitisha uamuzi wako kama ni sawa na Mungu anataka basi unahitaji kusoma na kuelewa neno la Mungu linaongoza vipi juu ya hili – maana limewekwa wazi katika biblia. Amri ya 8
Usifanye Uamuzi
utakaoleta mabadiliko katika Mabadiliko ni matokeo ya maamuzi ambayo ndani yake ‘yanadai’ mabadiliko fulani katika utekelezaji wake. Watu ambao hawapendi mabadiliko ni waoga kufanya maamuzi yanayoleta mabadiliko. Kwa mfano; uamuzi wa kuoa au kuolewa unaleta mabadiliko makubwa katika maisha ya mtu. Ukifanya uamuzi wa kuacha kazi unayoifanya kunaleta mabadiliko. Si mabadiliko yote ni mazuri au marahisi. Kuna mabadiliko mengine ni mabaya kwako. Tunachotaka ukumbuke ni hiki: maamuzi mengi ambayo mwanadamu anayafanya yanaleta mabadiliko. Je! uko tayari kwa ajili ya hayo mabadiliko? Amri ya 9 Usifanye uamuzi wowote bila lengo Ndiyo! Usifanye uamuzi wowote bila lengo! Hii ni kwa sababu uamuzi wo wote unaofanywa bila lengo unazaa matokeo yo yote. Uamuzi uliolengwa unazaa kilicholengwa. Hukuumbwa ili ufanye kila kitu, kwa hiyo usijiandae kufanya kila kitu. Badala yake chagua kufanya ulichoumbwa na ulichopakwa mafuta kukifanya. Amri ya 10 Omba Mungu akupe hekima yake ikusaidie kufanya maamuzi. Tuliumbwa ili tufanye maamuzi katika ulimwengu huu. Kwa hiyo jiandae kufanya maamuzi. Njia mojawapo ya kujiandaa ni kuomba Mungu akupe hekima kama alivyompa mfalme Sulemani. Hekima ndiyo iliyomsaidia mfalme Sulemani kufanya maamuzi yaliyomsaidia katika ufalme wake. Kufanya maamuzi ni mfumo wa maisha. Ukiogopa kufanya maamuzi huwezi kuishi vizuri, na utajikuta una maisha yasiyo na msimamo na mwelekeo mzuri na unaoeleweka. Mwisho Kufanya uamuzi ni uamuzi wako. Mungu hawezi kukulazimisha kufanya uamuzi, ila atakujengea mazingira ya kukusaidia ufanye maamuzi vizuri na mazuri. Usilaumu mzingira yaliyokufanya uamue ulichoamua kama hupendi matokeo ya uamuzi huo. Lazima uwajibike na matokeo ya maamuzi yako – ndio maana unahitaji msaada wa Mungu juu ya jambo hili la maamuzi. Mungu wetu azidi kukubariki na kukutunza. Tuzidi kuombeana. Ni sisi katika utumishi wa Kristo,
Christopher na
Diana Mwakasege |
|