INAWEZEKANA MUNGU AMEJIBU ILA JIBU
HALIJAJIDHIHIRISHA
BADO KWA SABABU YA UPINZANI.
Salamu katika Jina
la Yesu;
Kwa wale wanaosoma
biblia wanakumbuka habari za nabii Danieli alivyoomba kwa kufunga kwa
muda wa siku ishirini na moja "bila kupata jibu lo lote la Mungu"
Nabii Danieli
anatuambia hivi: " Katika siku zile mimi, Danieli, nalikuwa
nikiomboleza muda wa majuma matatu kamili. Sikula chakula kitamu, wala
nyama wala divai haikuingia kinywani mwangu, wala sikujipaka mafuta
kabisa, hata majuma matatu kamili yalipotimia" (Danieli 10:2,3).
Siku ya ishirini
na nne malaika Gabrieli alimtokea na kumwambia maneno haya: "Usiogope,
Danieli; kwa maana tangu siku ile ya kwanza ulipotia moyo wako ufahamu,
na kujinyenyekeza mbele za Mungu wako, maneno yako yalisikiwa; nami
nimekuja kwa ajili ya maneno yako. Lakini mkuu wa ufalme wa Uajemi
alinipinga siku ishirini na moja; bali, tazama, huyo Mikaeli, mmoja wa
hao wakuu wa mbele, akaja kunisaidia ..." (Danieli 10:12,13)
Nabii Danieli
alikaa kwenye maombi siku ishirini na moja, huku akidhani Mungu hajajibu
maombi yake. Lakini malaika Gabrieli alipomtokea katika siku ya ishirini
na nne alimwarnbia wazi ya kuwa maombi yake yalisikiwa na kujibiwa siku
ile ile ya kwanza aliyoanza kuomba.
Malaika Gabrieli
alimweleza Danieli jinsi ambavyo kutokana na kujibiwa rnaombi yake siku
ile ile ya kwanza, alitumwa aje amIetee majibu.
Ukifuatilia utaona
ya kuwa kati ya Danieli kuomba na Mungu kujibu rnaombi yake hakuna
tofauti ya siku wala kuchelewa. Maana Mungu alijibu maombi ya Danieli
siku ile ile ambayo Danieli aliomba!
Ila kati ya maombi
ya Danieli kujibiwa na majibu ya maombi kudhihirika kwa Danieli
kulikuwa na tofauti ya siku ishirini na nne!
Danieli angejua
toka siku ya kwanza ya kuwa maombi yake yamejibiwa asingeendelea kuomba,
bali angeendelea kumshukuru Mungu hadi majibu ya maombi yake
yamedhihirika kwake.
Hii huwa inatokea
mara kwa mara kwa watu wa Mungu wengi,ingawa wanakuwa ni wagumu
kulikubali. Mungu huwa anajibu rnaombi yao, na moyoni wanashuhudiwa
Mungu amejibu lakini hawaamini! Kwa nini? Kwa sababu hawajaona jibu
limejidhihirisha!
Lakini tunataka
tukutie moyo ya kuwa ikiwa umeomba jambo kwa Mungu, na moyoni
unashuhudiwa ya kuwa Mungu amekujibu ingawa 'kwa nje' bado jibu lenyewe
hujaliona -usikae mkao wa kutokuamini!
Wewe endelea
kumshukuru Mungu kwa majibu yake, na ikibidi endelea kumkemea shetani na
kumpinga sawasawa na Yakobo 4:7. Baada ya muda jibu lako
litajidhihirisha.
Inawezekana Mungu
amejibu maombi
yako lakini wewe hujui – na unadhani
Mungu amechelewa kukujibu!
Kuna mifano kadhaa
katika biblia ambayo Yesu alijibu maombi ya watu na wale watu wakapokea
majibu yao bila kwanza kuona majibu hayo kwa jinsi ya nje!
Mfano mmojawapo ni
wa yule mama wa kiyunani katika kabila ya Kisoforoinike.
Alikwenda kwa Yesu kuomba amponye binti yake ambaye alikuwa amepagawa na
pepo. Yule mama hakuwa amemchukua mtoto wake mgonjwa alipokwenda kwa
Yesu - alikwenda peke yake.
Yesu alimwambia;
"… enenda zako; pepo amemtoka binti yako" (Mathayo 9:29). Binti
mgonjwa hakuwa karibu nao Yesu alipotamka maneno hayo, na kwa hiyo
isingekuwa rahisi kwa yule mama kuyapokea maneno hayo ya Bwana Yesu kama
majibu ya maombi yake.
Lakini tunaona ya
kuwa yule mama, "akaenda zake nyumbani kwake, akamkuta yule kijana
amelazwa kitandani, na yule pepo amekwisha kumtoka" (Mathayo 9:29).
Huyu mama alifanya
kitendo cha kwenda nyumbani akiamini ombi lake lake limejibiwa ingawa
kwa macho halikuwa hajaliona hilo jibu hadi alipofika nyumbani.
Asingeyaamini maneno ya Bwana Yesu asingeondoka bali angabaki na
kuendelea kuomba. Au angetakata tamaa na kuogopa kurudi nyumbani kwa
mtoto wake. Lakini tunaona yule mama akifanya kitendo cha kwenda
nyumbani akionyesha kuwa aliyaamini maneno ya Yesu aliyosema juu ya
mtoto wake mgonjwa hata kabla hajayaona matokeo yaa maneno hayo kwa
macho.
Ndiyo maana
tunakwambia ya kuwa inawezekana Mungu amejibu maombi yako, lakini wewe
hujui, na unadhani Mungu amechelewa kukujibu. Je, umechukua hatua ya
kufuatilia eneo lile ulilotegemea jibu litokee ili ukaone kama limetokea
au la? Chukua hatua ya imani kama ya yule mama, nenda kamwangalie 'mtoto',
utamkuta amepona kama vile Yesu alivyosema.
Kumbuka Yesu
alipomjibu yule mama, hakumpa yule mama jibu la ombi lake ili ampelekee
mtoto wake, bali Yesu aliamua kulituma jibu la ombi la mama yule kwa
mtoto wake ambalo ndipo mahali lilipotakiwa kwenda. Yesu
akamwambia yule mama alichofanya, na kamwambia aende zake maana jibu la
ombi lake limetumwa lilikotakiwa.
Mfano mwingine
tunauona pale ambapo Yesu alimponya mtumwa wa akida mmoja kama
tunavyosoma habari hii katika kitabu cha Luka 7:2 –10.
Kama
ilivyokuwa kwa mama wa Kiyunani ndivyo ilivyokuwa kwa akida huyu. Jibu
lake lilitumwa moja kwa moja kwa mgonjwa naye akapona wakati akiwa mbali
na yule akida na wazee wa Kiyahudi waliomwombea kwa Yesu.
Yule akida ndicho
alichoomba! Maana alisema "…sema neno tu, na mtumwa wangu atapona"
(Luka 7:7). Yesu aliishangaa sana imani hiyo,.kwa sababu si wengi wanayo
imani ya jinsi hiyo, kwa kuwa wengi wanataka kuona jibu la maombi
yao kabla hawajaamini ya kuwa wamejibiwa! ‘Neno’ kwa wengi
halitoshi kuwa jibu la maombi yao!
Mfano mwingine ni
wakati Yesu alipomponya mtoto wa diwani mmoja bila mtoto huyo kuwa
karibu na mahali maombi yalipokuwa yanafanyikia.
Hali ya mtoto wa
diwani ilikuwa mbaya karibu na kufa, na akamwomba Yesu aende nyumbani
kwake amponye.
Badala ya Yesu
kwenda nyumbani kwa diwani, akamwambia diwani; "enenda,Mwanao yu hai"
(Yohana 4:50)
Yule diwani
angeweza kusita na kutokuamini na kuendelea kuomba au kuacha kuomba kwa
kukata tamaa. Lakini badala yake tunaona ya kuwa, "akalisadiki lile
neno aliloambiwa na Yesu, naye akashika njia" (Yohana 4:50). Na
alipofika nyumbani alimkuta mtoto wake mzima.
Cha ajabu ni
kwamba alipomkuta amepona aliwauliza wale waliokuwa wanamtunza mtoto
wake mgonjwa saa ambayo mtoto wake alipona! “ …. Wakamwambia, jana,
saa saba, homa ilimwacha. Basi babaye akafahamu ya kuwa ni saa ile ile
aliyoambiwa na Yesu, Mwanao yu hai” (Yohana 4:52,53).
Katika mfano wa
huyu diwani tunaona jinsi ambavyo tofauti kati ya yeye kujibiwa maombi
yake na yeye kuyaona majibu ya maombi yake ni siku moja nzima. Maana
alipofika nyumbani na kumkuta mtoto wake amepona na kuuliza saa
aliyopona, aliambiwa ni “jana, saa saba, homa ilimwacha”.
Je, maombi yako
yamejibiwa “jana” lakini hujui? Je! Umeulizia au umefuatilia huko
ulikotaka majibu ya maombi yako yadhihirike ili uone kama yamefika au
la?.
Unaweza ukawa unalalamika na kunung’unika kwamba Mungu
amechelewa kujibu maombi yako, na kumbe yalikwishajibiwa ‘jana’ na wewe
hujui!
Tuzidi kuombeana!