Yesu Akamwambia "Lisha Kondoo Zangu" (Yohana 21:17)
Home
Maombi
Ratiba
Shuhuda
Mafundisho
Maswali na Majibu
Barua za Mwezi
Kuchangia Huduma

Barua ya Mwezi Novemba 2005                                                            Kutoka kwa Christopher na Diana Mwakasege


BARUA YA MWEZI NOVEMBA 2005

Salamu katika Jina la Yesu Kristo.

            Toka Januari mwaka huu, kila mwezi tumekuwa tukikushirikisha kwa njia ya barua undani wa ujumbe wa kinabii ambao Mungu alitupa kuhusu Tanzania. Bado tuna mfano mwingine ambao ni vizuri pia upate kuufahamu.

Mfano wa
kanisa la Mwanzo

Unaposoma maisha ya kanisa la kwanza katika kitabu cha Matendo ya Mitume 2:43-47 unaona nini?

Mimi naona upako wa ukarimu (utajiri), ukijitokeza kabla ya upako wa watu wengi kuanza kuokolewa “kila siku”!

Habari kama hii unaiona tena unaposoma kitabu hicho hicho cha Matendo ya Mitume sura ya 4 na sura ya 5. Tunasoma kwa mfano ya kuwa: “Wala hapakuwa na mtu mmoja miongoni mwao mwenye mahitaji …kila mtu akagawiwa kwa kadri ya alivyohitaji”.

Uamsho wa utajiri ili kukidhi mahitaji katikati ya uamsho huo vilikwenda pamoja. La sivyo watu wengi wanaookoka watajikuta wana mahitaji mengi ambayo kanisa halina uwezo wa kuyatunza ipasavyo.

Lakini tizama hali ya kanisa la mwanzo! Kila uhitaji uliokuwepo ulitunzwa ipasavyo! Na moto wa injili ukaendelea vizuri na kwa muda mrefu!

Unadhani Mungu aliyewaidia wenzetu amebadilika? Au unadhani sisi tuna Mungu mwingine? La hasha!

Mungu ni yule yule! Yesu Kristo ni yule yule! Roho Mtakatifu ni yule yule! Kwa nini basi hata wakati huu uamsho mkubwa bado haujaja lakini kuna uhitaji na umaskini mkubwa katika watakatifu ambao kanisa linaonekana kutokuwa na ufumbuzi. Ikiwa hali iko hivi leo, je, ule uamsho mkubwa tunaoutarajia utokee katika nchi hii ukifika utakuwaje? Je! Unadhani Mungu ataacha uamsho atakaouleta ukose nguvu kwa sababu ya umaskini walio-nao watu wake?

Hapana! Mimi naamini Mungu aliyetuahidi ujio wake katika Tanzania ni mwaminifu, na aliyoahidi (utajiri na uamsho) atatuletea! Ikiwa alifanya mambo haya kwa wenzetu, basi, hata kwetu atatufanyia.

Jambo hili Mungu
anataka kulifanya tena!

Ndiyo! Jambo hili Mungu anataka kulifanya tena! Ikiwa aliwasaidia wenzetu hapa zamani, basi, na sisi atatusaidia, maana Yeye ni Mungu asiye na upendeleo!

Ikiwa alimsaidia Adamu katika bustani ya Edeni, basi, anaweza kutusaidia na sisi!

Ikiwa alimsaidia nabii Eliya, basi, anaweza kutusaidia na sisi pia!

Ikiwa alimsaidia nabii Eliya, basi, naweza kutusaidia na sisi pia.

Ikiwa alimsaidia Nehemia katika kuujenga ukuta wa Yerusalemu, basi, anaweza, na amekusudia kutusaidia na sisi pia!

Ikiwa alimsaidia mfalme Sulemani, kulijenga hekalu, basi, tuna uhakika hata leo atatusaidia na sisi pia!

Ikiwa kanisa lilipoanza liliona tabia hiyo hiyo, na udhihirisho huo huo wa Mungu, basi, tujue hata leo na sisi anaweza kutusaidia.

Hiki ni kipindi kizuri sana kwa ajili ya Tanzania. Neno hili limekuja kwetu ili kila anayelisikia apate kujiandaa ipasavyo juu ya ujio na udhihirisho wake.

Na ndiyo maana unahitaji kusoma na kutafakari na kutekeleza yaliyomo katika barua yetu ya mwezi ujao inayofuata.

Maranatha!!!!
 

UNATAKA KUOKOKA?
Kama unataka kumpa YESU maisha yako sasa, bonyeza hapa
©2003 Tanzania Social and Economic Trust.  All Rights Reserved.