Huduma ya Mana, wakishirikiana na kamati ya maandalizi ya Semina za Mwl Mwakasege Mkoa wa Kilimanjaro wanakuletea semina ya neno la Mungu katika mkoa wa Kilimanjaro, itakayofanyika kuanzia tarehe 25 Februari hadi tarehe 03 Marchi, 2019, katika uwanja wa mpira wa shule ya sekondari ya Majengo, kuanzia saa tisa alasiri hadi saa 12 jioni. Tunawakaribisha watu wote wakaazi wa Kilimanjaro katika semina hii, pia waleteni wagonjwa na wenye shida mbali mbali Yesu atawahudumia.