Maombi na maombezi kwa vijana

SEMINA YA VIJANA, UWANJA WA TANGANYIKA PARKES KAWE TAREHE 30 NOV - 01 DEC 2018:
Leo tunaendelea na semina ya vijana hapa uwanja wa Tanganyika Perkas Kawe tuliyoanza jana. Tunamshukuru Mungu kwa ajili ya semina ya siku ya jana, vijana wengi walihudhuria na tulikuwa na vipindi vya kumsifu Mungu, Maombi pamoja na Neno.

Jana Mwl Christopher Mwakasege, alitufundisha somo lenye kichwa kinachosema "UMUHIMU WA KUUNGANISHA AKILI NA NAFASI YA KUTUMIA AKILI HIZO". Katika somo hili ambalo lina lengo la "KUKUHIMIZA NDANI YA MOYO WAKO KUJIZOEZA KUOMBEA AKILI ZAKO ILI ZIWE MSAADA KWA TAIFA NA KWA UFALME WA MUNGU", tumejifunza kwa kuangalia mfano wa Yusufu mtoto wa Yakobo, kwenye biblia alivyopewa akili ambazo zilikuwa na manufaa kwa taifa la Misri na pia kwa ufalme wa Mbinguni. Leo tunaendelea na somo hili, nakukaribisha kijana kuja kusikilia na kulifanyia kazi somo hili.

SEMINA HII INARUSHWA LIVE KUPITIA:
1. Unaweza kusikiliza live kupitia kwenye tovuti hii kwa njia ya sauti tu, ingia sehumu ya MULTIMEDIA alafu fungua Broadcasting unaweza kutusikiliza liva kwa kutumia simu yako ya 'smartphone' au kwa computer yako.

2. Kupitia Redio Upendo FM ya hapa Dar es salaam ambayo inapatikana kwenye masafa ya FM, frequency namba 107.7

3. Kupitia Redio Wapo ya Hapa Dar es salaam inayopatikana katika masafa ya FM, Frequency namba 98.1.

Semina ya wanaume itafanyika tarehe 02 Disemba, kuanzia saa nane mchana mpaka kumi na mbili jioni.
Watu wote wanakaribishwa kushiriki semina hii, wagonjwa na wenye shida mbali mbali wataombewa na Yesu atawaponya na kukutana na shida zao.