|
|
| ||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
"Tena wahubirije, wasipopelekwa · · · " (Warumi 10:15a) "Ni askari gani
aendaye vitani wakati wowote kwa Kuchangia huduma za kupeleka Neno la Mungu kama tuliyonayo sisi – kwa fedha na/au kwa mali ni utaratibu ambao Mungu ameuweka, kwa sababu zifuatazo: 1. Kushiriki katika kupeleka Neno la Mungu Si wote wanaweza kupata nafasi ya kupeleka Neno la Mungu kila mahali wanapotaka lihubiriwe au lifundishwe. Na si kila mtu ameitwa kuhubiri au kufundisha kwa kusimama mbele za watu. Lakini unapotoa fedha au mali yako kusaidia kulipia gharama za kupelekea Neno, unakuwa ‘partner’ na anayepeleka Neno pamoja na Roho Mtakatifu anayewapeleka. Baraka zinazopatikana huko zinakufikia na wewe! 2. Ni njia mojawapo ya Mungu kukubariki kiroho na kimwili Yesu Kristo alisema, "Amin, nawaambieni, hakuna mtu aliyeacha nyumba, au ndugu waume, au ndugu wake, au mama, au baba, au watoto, au mashamba, kwa ajili yangu, na kwa ajili ya injili, ila atapewa mara mia sasa wakati huu, nyumba, na ndugu waume, na ndugu wake, na mama, na watoto, na mashamba, pamoja na udhia; na katika ulimwengu ujao uzima wa milele" (Marko 10:29,30) Mtume Paulo aliwaandikia wale waliokuwa wanachangia huduma yake akasema, "Na Mungu wangu atawajazeni kila mnachohitaji kwa kadri ya utajiri wake, katika utukufu, ndani ya Kristo Yesu" (Wafilipi 4:19) 3. Ni njia ya kuwasaidia watumishi wa Mungu wasilemewe na mzigo wa gharama za huduma na maisha yao ya kila siku. Ndiyo maana Mtume Paulo anauliza akisema, "Ni askari gani aendaye vitani wakati wowote kwa gharama zake mwenyewe?" (1Wakorintho 9:7). Kuna watumishi wengi wa Mungu ambao hawajafanya kazi ya Mungu gharama za huduma na za maisha yao ya kila siku na familia zao. Pamoja na Mungu kuwafungulia milango ya fedha moja kwa moja wao wenyewe, pia huwa anainua watu kwa ajili ya kuwasaidia. Yesu Kristo alisaidiwa pia! Ndiyo! Yesu Kristo alisaidiwa katika huduma yake na maisha yake alipokuwa hapa duniani!
Na Paulo naye alisaidiwa! Pamoja na kwamba Mtume Paulo alikuwa akifanya kazi ya kumsaidia kujitunza,(Matendo 18:1-3) tunaona ya kuwa Mungu alimwinulia watu wengi kumsaidia katika kueneza injili na katika maisha yake ya kila siku. Aliwaandikia Wafilipi akasema: "Nanyi pia, ninyi wenyewe mnajua, enyi Wafilipi, ya kuwa katika mwanzo wa Injili, nilipotoka Makedonia, hakuna kanisa lingine lililoshirikiana nami katika habari hii ya kutoa na kupokea, ila ninyi peke yenu. Kwa kuwa hata huko Thesalonike mliniletea msaada kwa mahitaji yangu, wala si mara moja · · · nimepokea kwa mkono wa Epafrodito vitu vile vilivyotoka kwenu, harufu ya manukato, sadaka yenye kibali, impendezayo Mungu" (Wafilipi 4:15 – 18) Kwa misaada hiyo Mtume Paulo alitumika katika huduma na kupata msaada wa mahitaji yake. Yeye alibarikiwa kwa misaada hiyo, na waliotoa walibarikiwa pia!(Wafilipi 4:19) Na sisi tunahitaji msaada wako! Ikiwa Yesu Kristo alisaidiwa, na Mtume Paulo alisaidiwa, na sisi ni vivyo hivyo! Tunahitaji msaada wa kutusaidia kuyafanya makusudi ya Mungu aliyotuwekea katika huduma na maisha aliyotupa. Tunamwomba Mungu aseme na wewe katika hili; na akumpe mzigo wa kutusaidia; na akufanikishe ili unapoongozwa na Roho Mtakatifu kutusaidia uwe na kitu cha kutusaidia. Kazi ya kupeleka Neno la Mungu si ya mtu mmoja. Tukisaidiana – inafanyika kwa nguvu, na kwa haraka na kwa upana zaidi. Tunamshukuru Mungu kwa wale ambao tayari wamekuwa wakitusaidia mara kwa mara kwa fedha na mali zao katika huduma tuliyonayo. Wamekuwa msaada mkubwa na washiriki wakubwa na neema na baraka tunazoziona kila siku katika huduma na maisha tuliyonayo. Kwa sasa huduma imepanuka na inaendelea kupanuka kwa haraka sana. Hii ina maana na gharama pia zinaongezeka. Lakini ashukuriwe Mungu katika Yesu Kristo anayelipia gharama za kazi anazoagiza zifanyike! Na katika kuzilipia gharama hizo anatumia watu walio na utayari wa kutii kama wewe! Tunaamini unatamani kama sisi kuona mafundisho ya Neno la Mungu na msaada wa Mungu unawafikia watu wengi na kwa haraka – Tanzania na pengine pote! Mungu ametupaka mafuta ya Roho Mtakatifu na kutupa nafasi ya kutumika kwa ajili hiyo. Tunahitaji msaada wako ili tuifanye kazi hii kwa haraka, na kwa ufanisi na kwa upana – kwa jinsi tuonavyo kurudi kwa Yesu Kristo kunavyozidi kukaribia. Unaweza kutoa msaada huo:
Ikiwa ni fedha tuma kwa akaunti iliyowekwa hapa chini: Jina la Akaunti: Christopher na Diana Mwakasege Nambari ya Akaunti: 01-J20-3221-4400 Jina la Benki: CRDB
BANK Kwa wanaotuma fedha toka nje ya nchi ya Tanzania pamoja na information hizo hapo juu ongeza SWIFT CODE zifuatazo: DEUTGB2L (kama unatuma fedha toka Uingereza) CITIUS 33 (Kama unatuma fedha toka United States of America) NBBKSESS (kama unatuma fedha toka Norway) KCBLKENX (kama unatuma fedha toka Kenya) NB:
? Ikiwa ni hundi andika kwa:
|
|