Utangulizi
JIFUNZE KUSAMEHE NA KUSAHAU
Tuna uhakika ya kwamba, Roho Mtakatifu anakuongoza kusoma somo hili kwa
makusudi kamili.
Maneno yaliyomo humu ni ya kukusaidia wewe na Wakristo wote, ili tuweze
kuishi maisha ya "amani na watu wote, na huo
utakatifu, ambao hapana mtu atakayemwona Bwana asipokuwa nao."(Waebrania
12:14).
Kusamehe na kusahau ni tatizo kubwa ambalo limewazuia wakristo wengi
wasipokee majibu ya maombi yao toka kwa Mungu. Ninaamini kuwa maneno
yaliyomo humu yatakusaidia katika kupokea majibu ya maombi mengi ambayo
hujayapokea.
Ni
maombi yetu kwa Mungu, katika Jina la Yesu Kristo ya kwamba, Roho
Mtakatifu ayachukue mafundisho haya na kuyaandika katika moyo wako, na
akusaidie kuyatenda.
Na
unaposoma itakuwa ni vizuri ukiwa na Biblia yako karibu, ili usome
mistari yote tuliyoiandika. Somo hili tutajifunza kwa wiki sita
mfululizo. Somo la wiki inayofuata litakuwa linajenga juu ya somo la
wiki linalotangulia hasa baada ya wiki ya kwanza.
Tutakuwekea
mfululizo wa somo hili kama ifuatavyo:
Wiki ya Kwanza:
Kutosamehe
ni kikwazo
Wiki ya Pili: Tabia
ya Mungu ya kusamehe ndani yako
Wiki ya Tatu: Hasara
za kulipiza kisasi
Wiki ya Nne: Hatua
Tano Muhimu katika kusamehe
Wiki ya Tano: Je!
aliyekukosea asipokuomba msamaha ufanyeje?
Wiki ya Sita: Utajuaje kama bado hujasamehe?
Tunataraji ya kuwa utaungana pamoja nasi kila wiki katika kujifunza somo
hili. Ni maombi yetu kwa Mungu ya kuwa somo hili litakusogeza hatua
nyingine muhimu katika maisha yako.
Jifunze
kusamehe na kusahau / Utang / 1 / 2
/ 3 / 4 / 5
/ 6 /