Utangulizi
NAMNA
YA KUWA MTENDAJI WA NENO
Katika
utangulizi fahamu mambo matatu makubwa yafuatayo:
1.
Wewe ni balozi wa Kristo na kwa ajili ya Kristo hapa ulimwenguni.
“Basi tu wajumbe (mabalozi) kwa ajili ya Kristo….” (2Wakorintho
5:20)
2.
Ikiwa wewe ni balozi, basi wewe si wa ulimwengu huu kama vile
Kristo asivyo wa ulimwengu huu (Yohana 17:16). Uraia wako au wenyeji
wako si wa hapa ulimwenguni, bali ni wa nyumbani mwake Mungu. “
Basi tangu sasa ninyi si wageni wala wapitaji, bali ninyi ni wenyeji
pamoja na watakatifu, watu wa nyumbani mwake Mungu.” (Waefeso
2:19)
3.
Ikiwa wenyeji wako ni mbinguni katika ufalme wa Mungu, nyumbani
mwake Mungu unafanya nini hapa ulimwenguni? Kuna sababu kubwa za wewe
kuwa hapa ulimwenguni. Ni kwa sababu umetumwa kama Kristo
alivyotumwa. “Kama vile ulivyonituma mimi ulimwenguni, nami vivyo
hivyo naliwatuma hao ulimwenguni.” (Yohana 17:18)
Tunajua
hukutumwa hapa ulimwenguni ili ufanye kazi peke yako. Tuko hapa
ulimwenguni tukiwa wafanyakazi pamoja na Mungu. “ Maana sisi tu
wafanya kazi pamoja na Mungu…” (1Wakorintho 3:9)
Huwezi
ukawa mfanyakazi pamoja na Mungu bila ya kuwa mtendaji wa Neno; kwa kuwa
Mungu ni Neno (Yohana 1:1). Kuwa balozi wa Kristo maana yake ni kuwa
mwakilishi wa Neno; kwa kuwa Kristo ni Neno (Yohana 1:14). Uwakilishi
huu hauonekani kwa sabatu watu wa Mungu walio wengi hawaelewi namna ya
kuwa watendaji wa Neno ili Neno lionekane hapa ulimwenguni.
Katika
somo hili tunajifunza juu ya namna ya kuwa mtendaji wa Neno, ili ufanye
kazi ya ubalozi wa Kristo vizuri. Ni maombi yetu kwa Mungu ya kuwa somo
hili lizae matunda katika maisha yako ya kiroho katika Kristo.
Wiki ya
Kwanza: Umuhimu
wa kuwa Mtendaji wa Neno
Wiki ya Pili:
Kuwa
Mtendaji wa Mungu ni sawa na kuiteka Nchi ya Ahadi
Kuwa
Mtendaji wa Neno / utang / 1 / 2
/