-
roho ya mpinga Kristo
ndiyo iliyoshambulia mafanikio ya kifedha katika watu wangu,
-
Imeelekeza
mashambulizi katika mafanikio ya roho zao (na nafsi zao) maana
nimesema mtafanikiwa katika mambo yote kwa kadri roho zenu
zifanikiwavyo,
-
Kufanikikiwa kwa roho
zenu kunategemea kufanikiwa kwa nafsi zenu. Mtafanikiwa katika roho
zenu kwa kadri nafsi zenu zifanikiwavyo, na matokeo yataonekana
katika mambo yote
-
Nafsi zenu
zifanikiwavyo zinategemea utendaji wenu wa Neno langu. Ikiwa
utendaji wenu wa Neno ukiwa hafifu, na kufanikiwa kwa nafsi zenu
kunakuwa hafifu. Kufanikiwa kwa nafsi zenu kukuwa hafifu na
kufanikiwa kwa roho zenu kunakuwa hafifu, kwa hiyo kufanikiwa katika
mambo yote kunakuwa hafifu pia.
-
Ndiyo maana nasema
roho ya mpinga Kristo imeelekeza mashambulizi yake katika kupinga,
kuzuia, na kuchelewesha mafanikio yenu katika roho na nafsi zenu.
-
Lakini mnaweza
kushinda kwa kusimama katika Neno langu ambalo ni upanga wa Roho
mikononi mwenu.
-
Nimesema katika Yoshua
1:8 ya kuwa mtafanikiwa ikiwa mambo matatu yatafanyika juu ya Neno
langu:
(a) Lisiondoke kinywani mwenu
(b) Mlitafakari wakati wote
(c) Na kudumu kulitenda
-
Sasa angalia
mmesimamaje katika maeneo hayo matatu. Maana hizo ni mbinu za
kulitumia Neno langu kama silaha ya kumshinda adui
-
Mkisimama katika Neno
langu ninavyotaka mtavuna mafanikio sana kwa wakati wangu msipozimia
na kukata tamaa katika mioyo yenu.
-
roho ya mpinga Kristo
inawakatisha tamaa kwa kuwaangaliza matokeo ya upungufu mlionao
badala ya kuangalia ahadi zangu na matokeo yake.
-
Kwa kadri
mnavyoangalia matokeo ya upungufu mlionao, ndivyo mnavyozidi
kutafakari juu ya upungufu mlionao. Kwa kadri mnavyozidi kutafakari
juu ya upungufu mlionao, ndivyo mnavyozidi kukiri na kushuhudia
upungufu mlionao na matokeo yake.
-
Kumbuka mnayafunga
mafanikio yenu kwa maneno ya vinywa vyenu yanayotoka katika nafsi
zisizotafakari ahadi zangu na matokeo yake.
-
Mimi si mtu hata
niseme uongo. Nililolisema katika Neno langu nimesema nitalitimiliza.
Napenda kufanikiwa kwenu kuliko nyinyi mnavyopenda kufanikiwa kwa
watoto wenu. Msikubali adui ayumbishe macho yenu na mioyo yenu
isione uaminifu wangu.
-
Mkisimama katika neno
langu na kupigana hivyo vita vizuri vya imani mlivyo navyo;
- mtashangilia ushindi wakati kuta
hazijaanguka bado,
- mtatangaza ushindi wakati bado upinzani wa adui umesimama,
- mtaona mafanikio wakati bado mmezungukwa na upungufu,
-
Kumbuka neno langu
linatangaza ushindi katika roho kwanza kabla ya haujaonekana kwa nje.
Ndicho kilimchomsaidia Ibrahimu wakati anasubiri mtoto wake. Na
ndicho kilichonisaidia na mimi pale masalabani - nilishangilia
ushindi dhidi ya adui hata kabla sijafufuka. Daudi naye aliuona
ushindi wakati bado Goliati amesimama mbele yake.