|
|
| ||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
KWA
NINI SI MAPENZI YA MUNGU TUWE MASKINI?
Nafahamu ya kuwa katika Mathayo 5:3, Yesu Kristo alisema; “Heri
walio maskini wa roho; maana ufalme wa mbinguni ni wao.” Watu
wengi wanapousoma mstari huu, wanadhani Yesu Kristo alisema “Heri
walio maskini wa mahitaji ya MWILI; maana ufalme wa mbinguni ni wao.”
Lakini Kristo hakusema hivyo.
Mtu maskini maana yake ni mtu mhitaji. Yesu Kristo aliposema “Heri
walio maskini wa roho …….” Alikuwa ana maana ya kusema
‘Heri walio wahitaji wa mambo ya rohoni; maana ufalme wa mbinguni ni
wao. Ndiyo maana aliongeza kusema, “Heri wenye
njaa na kiu ya haki; maana hao watashibishwa" (Mathayo 5:6).
Mtu
aliye maskini wa mambo ya mwili ni yule aliye mhitaji wa mambo ya mwili.
Na mambo ya mwilini ninayoyasema ni mavazi, chakula na mahali pa kulala.
Yesu Kristo hakusema heri wale walio na mahitaji ya chakula, mavazi,
afya na malazi.
Ninaposema
mahitaji ya mwili usije ukachanganya na matendo ya mwili yaliyoandikwa
katika Wagalatia 5:19-21 ambayo ni uasherati, uchafu, ufisadi, ibada ya
sanamu, uchawi, uadui, ugomvi, wivu, hasira, fitina, faraka, uzushi,
husuda na ulevi. Mimi siyazungumzii hayo ninaposema juu ya mahitaji ya
mwili. Mahitaji ya mwili ninayoyasema ni mavazi, chakula, nyumba na
matibabu.
Kwa
hiyo si sawa kabisa kwa mtu kuhalalisha umaskini wa mwili, yaani ukosefu
wa chakula, mavazi, matibabu na nyumba, kwa kutumia maneno ya Bwana Yesu
Kristo yaliyo katika Mathayo 5:3: Nataka
kurudia tena; si mapenzi ya Mungu mtu awe maskini.
Unaweza
ukaniuliza na kusema, “Bwana Mwakasege kama si mapenzi ya Mungu mtu
awe maskini, mbona basi kuna matajiri na maskini, je! Mungu hakuwaumba
wote?
Ni
kweli kwani hata imeandikwa katika Mithali 22:2, kuwa “Tajiri
na maskini hukutana pamoja; Bwana ndiye aliyewaumba wote”.
Lakini fahamu ya kuwa ingawa matajiri na maskini waliopo wote waliumbwa
na Mungu; tangu mwanzo wa uumbaji Mungu hakuyaweka matabaka haya mawili.
Hapo
mwanzo Mungu alipomuumba mtu, hakuweka ndani yake utajiri na umaskini
pamoja. Wala hakuumba watu wengine wawe matajiri na wengine wawe maskini.
Tunafahamu ya kuwa mtu aliumbwa kwa mfano wa Mungu na kwa sura ya Mungu.
Na naamini ya kuwa utakubaliana nami nikisema Mungu wetu si maskini kwa
hiyo hatukuumbwa kwa mfano wa kimaskini wala sura ya kimaskini. Ninazo
sababu nne ambazo ningependa kukushirikisha:
“
Bali utamkumbuka Bwana , Mungu wako, maana
Lakini fahamu ya kuwa si matajiri wote waliopo duniani wameupata utajiri
kutokana na nguvu walizopewa na Mungu. Wengi wamepata utajiri kwa njia
ya dhuluma. Na ndiyo maana sehemu nyingi katika Biblia matajiri wa jinsi
hiyo wamekemewa. Soma Amosi 5:11, 12. Kwa sababu hii Mungu hayuko upande
wa matajiri hawa. Hii pia haimaanishi kuwa Mungu yuko upande wa KILA
maskini aliopo duniani. La hasha! Mungu yuko upande wa yule
ayafanyaye mapenzi yake awe tajiri au maskini (Mathayo 7:21)
Watu wengi wametajirika kwa njia ya rushwa na kutokusimamia haki pamoja
na uchoyo. Na hii si sawa hata mbele za Mungu. Ni dhambi zilizo wazi
kabisa. Na wote wafanyayo hayo wanahitaji kutubu!
Ngoja nikueleze jambo muhimu: Mungu anapokupa nguvu za kupata utajiri,
anakupa akiwa na lengo na kusudi muhimu.
Imeandikwa,
“………. Ili alifanye imara agano lake alilowapa baba zako, kama
hivi leo”
Kwa kuwa tu kuna matajiri wasio wa haki basi haimaanishi kuwa matajiri
wa haki hawapo. Ni budi tuweze kutofautisha utajiri ulio wa haki na
utajiri usio wa haki.
Mungu
wetu tunayemwabudu na kumtumikia katika Kristo Yesu si Mungu wa hasara
bali Mungu wa faida. Imeandikwa hivi;
Watu wengine kwa kutokuwa wavumilivu, na kutokujali mafundisho ya Mungu;
wameamua kujipatia faida kwa kuwadhulumu, kuwakandamiza na kuwanyonya
wengine. Na inasikitisha jinsi wanavyomshirikisha Mungu katika faida
najisi namna hiyo waposema ya kuwa ni Mungu aliyewasaidia ‘kudhulumu
na kunyonya’. Ni wazi ya kuwa Mungu hakuwasaidia kupata faida kwa njia
ya udhalimu.
Na pia ukisoma katika Hagai 2:8 unaona imeandikwa hivi “Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema Bwana wa majeshi” Ngoja nikuulize swali; Je! unadhani vitu vyote hivi Bwana amemwekea nani? Unadhani alimwekea shetani na watu wanyonyaji wachache? La
hasha!
Nadhani kuwa kuna wakristo wengi ambao wana mawazo kama haya. Ni kweli
kwamba Yesu Kristo alipokuwa hapa duniani alikuwa maskini. Lakini hakuwa
maskini ili sisi tuwe maskini; bali alikuwa maskini ili sisi tuwe
matajiri! Kama alikuwa maskini ili sisi tuwe maskini kama wengine
wanavyodhani, basi kazi hiyo haina faida kwetu. Lakini Yesu Kristo
asifiwe kwa kuwa alikuwa maskini ili sisi tuwe MATAJIRI.
Na ndiyo maana alisema katika Luka 4:18a ya kuwa;
“Roho wa Bwana yu juu yangu, kwa maana amenitia mafuta kuwahubiri
MASKINI habari njema.”
Mtume Petro naye aliwahi kusumbuliwa sana na jambo hili, hata ikabidi amuulize Bwana Yesu.
“Ndipo
Petro akajibu, akamwambia, tazama, sisi tumeacha vyote tukakufuata,
TUTAPATA NINI BASI?” (Mathayo 19:27)
Kumbuka ya kuwa; Yesu Kristo alichukua dhambi zetu na akafanyika dhambi
kwa ajili yetu, “ Ili sisi tupate kuwa haki ya
Mungu katika Yeye” (2Wakorintho 5:21). Na kwa kujua hili kanisa
linahubiri habari za ondoleo la dhambi kwa yeyote atakayemwamini Kristo. |
|