Yesu Akamwambia "Lisha Kondoo Zangu" (Yohana 21:17)
Home
Maombi
Ratiba
Shuhuda
Mafundisho
Maswali na Majibu
Barua za Mwezi
Kuchangia Huduma
MAOMBI YA NCHI


Maombi ya kuombea Nchi

Wiki ya Tano:

1.      Ombea vijana wa Tanzania Mungu awalinde awaokoe na mitego ya adui
-         
ulevi – wa pombe na madawa
-         
wawe na mwelekeo mwema na malengo katika maisha
-         
Mungu awaepushe na tamaa mbaya ya vishawishi
-         
Mungu awape hekima ya kuchuja baya na jema wasiige tu vitu

2.      Omba Tanzania kukaa katika mpango na kusudi la Mungu.

3.      Ombea huduma mbalimbali za jamii Tanzania ziboreshwe.
Ombea barabara za
Tanzania mijini na vijijini zitengenezwe ziwe za kisasa ziweze   kutumika majira yote ya mwaka.

Wiki ya Nne:

1.      Ombea uchaguzi wa rais na viongozi wa serikali mwakani 2005
-         
Uchaguzi wote kwa ngazi zote utawaliwe na Roho Mtakatifu
-         
Mungu awaandae wale aliowakusudia na kuwapitisha
-         
Uchaguzi uwe wa haki, amani na kweli
-         
Wale wote wanaotegemea nguvu za giza, hongo na hila zozote na wenye mipango na malengo   mabaya wasichaguliwe, wasipite.
-         
Gharama za maandalizi na uchaguzi ziwe za kiasi na haki
-         
Ombea katiba ya nchi (ya uchaguzi, muungano)
-         
Ombea mfumo wa siasa nchini – Mungu aratibu

2.      Ombea mikataba mbalimbali Tanzania inayoingia ya kibiashara, elimu, kiserikali n.k ili Mungu achuje na kuiepusha nchi na mikataba ya hila na yenye mitego.
-         
Ombea balozi zetu
-         
Ombea mahakama za Tanzania – haki itendeke
-         
Kemea roho ya rushwa Tanzania

3.      Ombea sekta ya elimu nchini
-         
Watanzania wawe na moyo wa kuthamini na kupenda elimu na kupenda kujiendeleza kielimu.
-         
Mfumo wa elimu inayotolewa umsaidie mtanzania hapa nchini na hata nje ya nchi
-         
Vyuo ambavyo havifanyi kazi kwa ngazi iliyokusudiwa vianze (vifufuke) kutumika ipasavyo
-         
Mashule na vifaa vya kufundishia vipatikane
-         
Walimu, wakufunzi walipwe vizuri, wawe na moyo wa kujituma

Wiki ya Tatu:

1.      Omba hekima ya Mungu kwa viongozi wa ngazi zote hapa nchini kwenye kanisa, serikali, vyama na mashirika mbalimbali wawe na hofu ya Mungu, kiasi, moyo wa kujituma na uaminifu.

2.      Ombea hali ya:
-         
Mvua zinyeshe kwa majira yake na zakutosha bila madhara
-         
Vyanzo vya maji visikauke na utunzaji wa mazingira
-         
Mungu atuepushe na majanga ya ukame, mafuriko, vimbunga, tufani, na matetemeko ya ardhi, moto.

3.      Mungu atuepushie tauni mbaya, macho ya watanzania yafunguke na kuona sawasawa ili kuepukana na magonjwa mabaya.
-         
ukimwi
-         
kipindupindu
-         
malaria
-         
misaada inayotelwa iwafikie walengwa (wagonjwa)

Wiki ya Pili:

1.      Omba ulinzi juu ya nchi ya Tanzania na mipaka yake yote izingirwe kwa  damu ya Yesu:
– Ulinzi kwa Rais wa Tanzania.

-      
Ulinzi kwa serikali na uongozi wote, ngazi zote
  -         
Ulinzi kwa mwili wa Kristo Tanzania (Kanisa)
  -         
Ulinzi katika njia kuu za usafiri na vyombo vinavyotumika (ndege, magari, maji n.k)
  -         
Ulinzi kwa vitu vinavyoingia nchini na kutoka – visiingie vile vitakavyoleta madhara vivyo na
             vinavyotoka. Ushuru usikwepwe kwa hila.

  -         
Ombea mawaziri, wakuu wa mikoa, wilaya na Bunge
 
-          Omba amani na utulivu ndani na nje ya Tanzania

2.      Kataa kwa jina la Yesu kila aina ya umwagaji damu Tanzania
-         
kwa njia ya ajali mabarabarani
-         
kwa vita
-         
kwa ibada za kishetani/kafara

3.      Omba Tanzania idumu kuwa mikononi mwa wa Tanzania. Uchumi ukue na kunufaisha watanzania kwa mfano madini, utalii
-         
Mungu ainue watu watakaosimamia kwa uaminifu maswala ya uchumi hapa nchini na kwa uongozi wake.

Wiki ya Kwanza:

1.      Shukrani   – kwa ajili ya nchi nzuri, amani iliyopo, uhuru wa kuabudu.

2.      Toba       
– Kanisa kutokusimama katika zamu ipasavyo, kulalamika
- Mambo yote yanayofanyika nchini yaliyochukizo kwa Bwana.

3.      Kufuta laana zote za maneno juu ya nchi hii, na kufuta dua zote mbaya kwa damu ya Yesu. Teka nyara anga la Tanzania na kulikabidhisha kwa Roho Mtakatifu atawale, kemea na kuharibu kazi zote za nguvu za giza.
- Roho wa maombi ashuke kwa kanisa la
Tanzania kwa ajili ya nchi.

 

UNATAKA KUOKOKA?
Kama unataka kumpa YESU maisha yako sasa, bonyeza hapa
©2003 Tanzania Social and Economic Trust.  All Rights Reserved.