|
|
| ||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
Ndugu katika Kristo, Naamini kuwa umefungua ukurasa huu kwa sababu una huduma ya maombezi na una mzigo wa kuombea wengine wenye shida na mahitaji mbalimbali. Tunakukaribisha ujiunge na Mailing List ya maombezi itakayokuwezesha kupata, kwa njia ya email, mahitaji na shida mbalimbali zinazohitaji huduma yako ya maombezi. Mailing List ni mtandao wa mawasiliano kupitia barua pepe yaani email. Kujiunga ni rahisi sana.
Inahitajika email address yako tu. Namna ya kujiunga:
1. Tuma email kwa "maombi-request@kicheko.com" 2. Usiandike chochote katika sehemu ya "Subject" 3. Sehemu ya ujumbe andika "subscribe" 4. Halafu itume. Komputa
itasoma na kutambua email address yako, itakuunganisha na kukupa majibu
papo hapo.Kama unataka kumuunganisha rafiki yako katika hatua ya 3 baada ya neno "subscribe" andika email address ya rafiki yako. Kwa mfano kama email address yake ni rafiki@kicheko.com basi katika hatua ya tatu hapo juu utaandika "subscribe rafiki@kicheko.com. Komputa itamtumia ujumbe wa kumtaka athibitishe. Kwa kujiunga na mtandao huu utapata emails zenye mahitaji ya maombezi na unachotakiwa kufanya ni kuwaombea ndugu hao sawasawa na mahitaji yao. Mungu akubariki sana. |
|