|
MAMBO YA
KUTAFAKARI KABLA YA KUFANYA
UAMUZI WA KUOA AU KUOLEWA
Wiki ya
Saba
Jambo
la Saba
Je! Uko
tayari kuoa au kuolewa?
Ni swali
muhimu, uko tayari, maana yake umefika mahali hali yako ya ndani
na nje, inakuruhusu kuoa au kuolewa? Uko tayari kuoa au kuolewa?
Umefika mahali pa namna hiyo?. Wengine wanasema huyu ni mtoto,
lakini unajua pamoja na kwamba ni mtoto, ni vizuri kujua kama
uko tayari kiumri. Lakini ninapozungumzia hapa juu ya utayari
wa kuoa au kuolewa, sizungumzii tu habari za miaka, bali
ninazungumzia habari za hali yako ya ndani.
Nimeona
kuna mtu mwingine ana miaka arobaini, lakini kwa kweli hayuko
tayari kukaa na mwanamke, ndani yake, mawazo yake na kufikiri
kwake, hayuko tayari kukaa na mwanamke, hawajibiki hata yeye
mwenyewe juu yake mwenyewe. Wengine hata wana miaka hamsini,
lakini ana hali kama hii. Nimeona akinadada hata wana miaka
arobaini na tano, hayuko tayari kuolewa, maana akiolewa ni shida
tu.
Nilienda
mahali fulani, nikakuta dada ana umri mkubwa tu, lakini wakati
wa maombi hakusema kama anataka tuombe ili aolewe. Nikaona ngoja
nimuulize labda anaona aibu kusema hitaji hili kwa sababu umri
umesogea, nikamwambia “hutaki tuombe uolewe”? Akasema, “hapana,
sitaki kuolewa” (Na alikuwa ana umri wa miaka kama arobaini na
zaidi). Nikamuuliza, “kwa nini”. Akasema, “kwa sababu sitaki
kuomba ruhusa kwa mwanaume ninapotaka kutumika”. Nikamuuliza
unafanya kazi, akasema, “ndio”.
Nikamwambia, “unapokwenda kumtumikia Mungu huwa unafanyaje, -
unaomba ruhusa au unatoroka huko kazini?” Akasema, “ninaomba
ruhusa”. Nikwamwambia, “kwa nini unaona ni rahisi kuomba ruhusa
kwa mwajiri wako na unaona taabu kuomba ruhusa kwa mume wako?”
Alishindwa kujibu hilo swali. Nikamwambia tatizo lako ni kubwa
kuliko unavyo fikiri.
Unaweza
ukaona kabisa ya kwamba, huyu mtu hayuko tayari kuolewa, wala
msijaribu kumlazimisha aoelewe – pamoja na kwamba umri wake ni
mkubwa. Usijaribu kumsukuma kwenye maamuzi ya kuolewa maana
hayuko tayari kuolewa, akiingia kwenye ndoa atakwenda kuleta
shida tu!
Ndio
maana ninakuuliza swali, je uko tayari kuoa au kuolewa? Lina
vipengele vingi vya kulitazama, na linabadilisha vitu vingi sana.
Mwingine
unakuta ni msichana, wazazi wake ndio wanamtegemea karibu katika
kila kitu. Mimi ninakuambia kabla hujafikiria kuoa au kuolewa,
fikiria hilo swali. Kwa sababu ukiishaolewa tu biblia inakuambia
wasahau watu wa nyumbani mwa wazazi wako (Zaburi 45:10). Sasa
haimaanishi usiwasaidie, ila maana yake ni kwamba huwezi
ukawasaidia tena ‘moja kwa moja’ kama ulivyokuwa unawasaidia
zamani. Ni vitu lazima ujadiliane na mume wako juu ya kuwasaidia
wazazi wenu wa pande zote mbili – maana mna mipango yenu sasa.
Na
inawezekana labda umeoa au umeolewa kwa kijana ambaye hana mzigo
na wazazi wake kabisa, kila mtu anaishi kivyake vyake kama simba
porini, suala la kusaidia wazazi hana ndani ya moyo wake. Wewe
umekuwa na huo mzigo, wazazi wako wamekulea, umefika mahali
umeanza kazi, sasa na wewe unawatunza hatua kwa hatua, siku
unaolewa yule baba anasema basi usiwatunze tena, - fikiri hilo.
Litakuwa
linakuumiza kila siku jinsi wazazi wako wanavyopata shida.
Utafika mahali utakuwa unachukua vitu kisiri siri unapeleka kwa
wazazi, na hiyo ina shida yake pia. Kwa hiyo kabla hujakubali
kusema mimi nataka kuolewa, fikiri kwanza na kuomba, maana ndoa
inakwenda kukubadilishia mambo yako mengi.
Mambo ya
Kutafakari Vijana / utang / 1
/
2 / 3 / 4 /
5 / 6 /
7 /
8 /
9 /
10 /
11 /
|