|
MAMBO YA
KUTAFAKARI KABLA YA KUFANYA
UAMUZI WA KUOA AU KUOLEWA
Wiki ya
Tisa
Jambo la Tisa
Uko tayari
kuoa au kuolewa lini, maana yake ni
muda gani ambao ungetaka kuoa au kuolewa?
Utasikia
mwingine anasema, siku Mungu atakapo nipa mume au mke, hii ni
hatari sana! Biblia inasema kwenye kile kitabu cha Mhubiri.3:1 “Kwa
kila jambo kuna majira yake na wakati kwa kila kusudi chini ya
mbingu”.
Kila kitu
kilichoko chini ya mbingu kimeratibiwa, kwa lugha nyingine, ni
kwamba kila mwanadamu ana kalenda yake, iko kalenda yako ya
kuzaliwa, na ipo kalenda ya matukio na mipango mbalimbali.
Mungu anaijua. Mungu anatangaza mwisho tangu mwanzo, anajua
mwisho wa maisha yako wakati wewe unapozaliwa.
Katika
mwanzo wa maisha yako, Mungu anakuwa amekwishajua mwisho wako;
utakavyokuwa; na kama amekwishajua mwisho wako, maana yake
ameshatembea kwenye maisha yako yote toka mwanzo mpaka alipofika
mwisho, na alipokamilisha maisha yako akarudi mwanzo ndipo
akakuongoza kuzaliwa.
Mungu
anapokuacha uzaliwe duniani, hakika ujue kabisa ya kwamba
amekwisha tembea na wewe katika maisha yako, amesharatibu mambo
yako na yako hatua kwa hatua; kwa mfano, kitu gani utafanya,
wapi utasoma, utasoma nini, utaolewa na nani au utaoa nani na
itakuwa, lini, maisha yako yatakuwaje, utamtumikiaje, mpaka
mwisho wako. Akiishafika mwisho wa maisha yako anarudi mwanzo,
akishafika mwanzo anatangaza mwisho tangu mwanzo; kwa hiyo
kuanzia hapo unapozaliwa ujue maisha yako yote yamesharatibiwa!
Ni vizuri
ufahamu hii mistari itakusaidia, maana inakujengea msingi mzuri
wa maisha hapa. Isaya.46:9-10 inasema, “Kumbukeni mambo ya
zamani za kale maana mimi ni Mungu wala hapana mwingine, mimi ni
Mungu wala hapana aliye kama mimi. Nitangazaye mwisho tangu
mwanzo, na tangu zamani za kale mambo yasiyotendeka bado,
nikisema, shauri langu litasimama, nami nitatenda mapenzi yangu
yote”.
Kwa lugha
nyingine anatuambia ya kwamba, ‘wewe unaona kila kitu ni kipya,
unapoishi kila siku ni mpya, kila dakika inayokuja ni mpya,
Mungu anasema hiyo safari unayopita, mimi nilikwishaipita tayari,
nikafika mwisho wa maisha yako ndipo nikakuruhusu uzaliwe.
Ulipokuwa unazaliwa nikatangaza mwisho wako tangu wakati
unazaliwa.
Sasa mimi
ninataka nikuambie kama Mungu anajua, na shauri lake anasema
litasimama katika maisha yako, ili mapenzi yake ayatende katika
maisha yako, unahitaji kuwa mwangalifu. Kwa sababu kuna mpango
na saa ya Mungu ya kuoa au kuolewa, - ipo!
Mungu
anapokuletea mawazo ya kuoa au kuolewa, ni kwa ajili
yakuimarisha maisha yako na wito wako na kazi na makusudi,
ambayo ameyaweka hapa duniani. Atakuletea mtu atakaye imarisha
wito wako, atakuletea mtu atakaye saidiana na wewe, uwe ni
mwanamke au uwe ni mwanaume.
Mungu
anapo kukutanisha na mtu wa kuoana naye ni kwa ajili ya
kuimarisha nguvu zenu ili mtimize kusudi la Mungu. Kwa hiyo
lazima anajua kuna saa huyu mvulana anahitaji mke, au huyu
msichana anahitaji mume! Lakini watu wengi sana hawalifuatilii
hili. Wakati sisi tunaoana na mke wangu tulikuwa bado vijana,
tulioana hatujafikisha hata miaka thelathini, ninakumbuka
nilikuwa na miaka 28. Tulijaliwa kuwapata watoto tungali bado
vijana sana. Lakini tuna watoto ambao ni wakubwa kwa sasa.
Tumefika kipindi ambacho tunaweza tukafuatilia masuala ya
utumishi kwa namna ambayo haiwaumizi watoto wetu sana!
Maana
watoto wakiwa wadogo wote, mimi ninakuambia kumtumikia Mungu ni
kunakuwa kugumu sana, usije ukafikiri ni kurahisi. Maana
unahitaji kuwa karibu nao; wanahitaji kusoma shule, wanahitaji
kufanya vitu mbalimbali, wanahitaji kuwa na baba karibu,
wanahitaji kuwa na mama karibu. Saa nyingine mnataka kusafiri
nao; unaweza ukasafiri nao lakini usije ukafikiri ni kitu
kirahisi.
Tulisafiri
na Joshua (mtoto wetu wa nne) akiwa na wiki sita. Sijawahi kuona
watu wakisafiri na watoto wao wakiwa wadogo namna hiyo, Joshua
alikwenda kwenye huduma akiwa na wiki sita tu. Hatukuwa na namna
ambavyo tungeweza kumwacha. Sasa unaweza ukaelewa akiwa na wiki
sita; maana yake mama yake ana muda wa wiki sita tu tangu
ajifungue na tulisafiri kwa gari, sio kwa ndege, bali kwa gari!
Tulisafiri
masaa karibu kumi na mbili, tumebeba kila kitu, tumebeba mpaka
unga wa kutengenezea uji, na beseni la kuogea, na maji. Huwezi
kumwogeshea mtoto mchanga wa wiki sita maji yoyote tu, kwa hiyo
tulibeba maji ya kumwogeshea. Huwezi kwenda ‘spidi’ unayotaka,
ikifika saa yake ya kula lazima usimame! Ukifika kwenye hoteli
huwezi kumlaza jinsi unavyotaka, lazima uingie kwanza uombe,
uangalie yale mashuka yaliyoko halafu uombe, uangalie kile
kitanda halafu uombe, uangalie kila kitu kule ndani halafu uombe!
Wewe ni
mtumishi wa Mungu, ukienda na mtoto kienyeji kienyeji tu,
ibilisi anaweza akamvamia na ukapata shida, na huduma yako yote
uliyoiendea ikaharibika. Unaweza ukatamani saa nyingine usinge-
safiri naye. Lakini mnaposafiri pamoja, kumbuka ina gharama yake.
Lakini
mambo haya unahitaji kufiri mapema, ili uweke kwenye agenda
yako ya maombi ujue kabisa mpango wa Mungu ya kuwa unatakiwa
kuoa au kuolewa lini. Ninajua kwa wengi kinakuwa kigumu hicho,
maana wengine wametamani kuolewa jana, hawajapata wanaume,
wengine wangetaka kuoa leo, lakini bado hawajapata msichana wa
kuoa.
Wengine
wanatamani kuolewa si kwa sababu mpango wa Mungu umefika wa
kuolewa; ila ni kwa sababu wanaona muda wao wa kuolewa umefika,
wengine wanaona umri umesogea. Mpango wa Mungu juu ya maisha
yako, haubabaishwi na jinsi wewe unavyohesabu miaka,jirani zako
wanavyohesabu miaka, ndugu zako wanavyohesabu miaka, au rafiki
zako wanavyohesabu miaka.
Mungu
anajua alichopanga kwa ajili yako, ana kalenda yako kabisa, na
kila alichokichagua Mungu ndicho sahihi.
Mambo ya
Kutafakari Vijana / utang / 1
/
2 / 3 / 4 /
5 / 6 /
7 /
8 /
9 /
10 /
11 /
|