|
MAMBO YA
KUTAFAKARI KABLA YA KUFANYA
UAMUZI WA KUOA AU KUOLEWA
Wiki ya
Kumi na Moja
Jambo la Kumi na Moja
Uko tayari
kuishi katika hiyo ndoa kwa muda gani?
Sasa ninakupa siri hapa ikusaidie, Kama umekaribia – karibia
kuoa au kuolewa, na hujawahi kujiuliza maswali ya namna hii,
basi Mungu anakuweka mahali pazuri kwa kukupa nafasi ya kusoma
kitabu hiki. Labda nikuambie kitu cha namna hii kitakusaidia,
kabla sijakupa mistari mingine kwenye biblia, ni hivi: Hakuna
sababu ya kuolewa na kijana ambaye atakufa baada mwezi mmoja. Au
hakuna sababu ya kuoa msichana atakayekufa muda si mrefu baada
ya arusi yenu.
Kwa nini
uolewe leo uwe mjane baada ya miezi miwili? Na ukiishaolewa
umekwisha badilisha kabisa hali yako na ya mume wako; akiisha
kufa wewe sio msichana tena, utaitwa mjane, hata kama umri wako
ni mdogo. Tulienda mahali ulani tukasema tunaomba wajane
tuwaombee, tulishangaa kuona ya kuwa robo tatu yao walikuwa ni
wasichana. Ungeambiwa wameolewa ungekataa, lakini wamefiwa bado
wana umri mdogo.
Sasa mimi
ninataka nikuulize swali, kwa nini unataka uolewe, halafu mume
wako afe baada ya miezi miwili au unataka uoe mke wako afe baada
ya mwezi mmoja, au baada ya mwaka? Hakuna kitu kinachosumbua
kama hiki. Ngoja nikueleze hili tena ya kuwa ndoa ya pili sio
ndoa ya kwanza. Ndoa ya kwanza ina utofauti wake, na ndoa ya
pili ina utofauti wake.
Ikiwa
unataka kuishi muda mrefu na mwenzi wako wa ndoa unahitaji;
1.
Kuwa
mwangalifu kutii ile mistari ilioko kwenye biblia inayozungumzia
juu ya muda wa mtu kuishi. Kwa mfano: Waefeso 6:1-3 inasema;
“Enyi watoto, watiini wazazi wenu katika Bwana, maana hii ndiyo
haki. Waheshimu baba yako na mama yako; amri hii ndiyo amri ya
kwanza yenye ahadi, upate heri, ukae siku nyingi katika dunia”.
Kwa hiyo
angalia uhusiano wako na wazazi wako kama bado wako hai. Lakini
pia chunguza uhusiano wa huyo anayetaka kukuoa au anayetaka
umuoe, na wazazi wake, kama bado wako hai.
2.
Omba Mungu akupe maisha marefu na huyo mwenzako hata
kabla hamjaamua kuoana. Ili kama kuna mmoja wenu hataishi muda
mrefu – basi Mungu awaarifu na kuwaongoza cha kufanya.
Mwingine
anataka aingie kwenye ndoa kwa kubahatisha au kwa majaribio.
Maana yake ndani ya nafsi yake anajiweka tayari kuachana na
mwenzi wake kama anaona mambo ya ndoa yake hayaendi
alivyotarajia. Mtu wa namna hii hataweza kuwa mvumilivu na
mwepesi wa kutafuta suluhisho kukitokea tatizo katika ndoa yake.
Uamuzi wa
kuoa au kuolewa unamtaka mtu aingie katika ndoa asilimia mia
moja. Ikiwa hautakuwa tayari kuingia kwenye ndoa kwa asilimia
mia moja – tafadhali usiamue kuoa au kuolewa. Utampotezea tu
mwenzako – maana hakuna ndoa isio na matatizo. Lakini pia hakuna
tatizo ambalo Mungu hawezi kulitatua. Lakini, je, uko tayari
kushirikiana na Mungu katika ndoa kwa kiwango cha asilimia ngapi?.
Mambo ya
Kutafakari Vijana / utang / 1
/
2 / 3 / 4 /
5 / 6 /
7 /
8 /
9 /
10 /
11 /
|