Tunamshukuru Mungu kwa mwaka huu, kuanzia tarehe 23 hadi 26 July 2019 tumekuwa na Kongamano la maombi la Kitaifa, lililofanyika katika chuo kikuu cha UDOM. Katika Kongamano hili kama yalivyokuwa Makongamano mengine yaliyotangulia, tulipata nafasi ya kuwa na waombaji toka kila wilaya ya nchi yetu, na baadhi ya waombaji toka mataifa ya jirani kama Kenya, Burundi, Kongo, Zambia, Marekani na Uingereza.

Tunamshukuru Mungu kwamba tulikuwa na agenda mbalimbali za maombi kwa ajili ya kuiombea nchi yetu, na siku ya tarehe 25 July 2019 tuliitangaza kama siku ya maombi ya kitaifa, ambapo tuliungana na redio tofauti tofauti hapa nchini pamoja na television ya Upendo kuungana na watanzania wengine nchi nzima.