Salamu katika jina la Yesu!

Tunamshukuru Mungu sana kwa jinsi ambavyo amekupa kuifuatilia huduma yetu kwa karibu, na kwa kuendelea kutuombea.

Mwezi uliopita wa Mei tulikuwa na semina Singida mjini tarehe 1 – 5 mei, halafu tukawa na semina mbili nchini Marekani – tarehe 24 – 26 mei mjini Minneapolis, Minnesota na tarehe 31 Mei hadi 2 Juni mjini Dallas, Texas.

Tunamshukuru Mungu sana kwa ushindi mkubwa uliopatikana katika semina zote hizo. Sifa na heshima tunamrudishia Kristo Yesu, ambaye pasipo Yeye sisi wenyewe tusingeweza kufanikisha chochote.

Mwezi huu wa Juni tuna safari ya Israeli ya kimafunzo tarehe 12 – 21, na baada ya hapo tutakuwa na semina Morogoro mjini tarehe 25 – 30.

Na mwezi ujao wa julai – tunatarajia kuwa na kongamano la maombi la kitaifa tarehe 9 – 12 na baada ya hapo tunatarajia tuwe na semina ya neno la Mungu Mwanza mjini tarehe 21 – 28.

Ujumbe tulionao kwako mwezi huu ni kwamba: Utoaji wako wa sadaka uimarishe pia uhusiano wako na Mungu.

Mungu alipokuwa anazungumza na Kaini baada ya kumkataa na kuikataa sadaka yake; alimwambia: “Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko…” (Mwanzo 4:7).

"…Usipotenda vyema dhambi iko ….", hapa ina maana ya usipotenda kwa Imani, hasa unapoulinganisha mstari huu na ule wa Waebrania 11:4. Kilichomfanya Kaini asipate kibali katika utoaji wake wa sadaka ni kwamba hakutoa kwa Imani, kama Habili alivyofanya.

Kufuatana na Warumi 10:17 na Waebrania 11:1 tunaelewa ya kuwa, Imani ni matokeo ya Mungu kumpa mtu maelekezo juu ya jambo la kufanya; huku maelekezo hayo yakiunganishwa au yakiambatanishwa na matarajio, ikiwa utatekeleza ipasavyo maelekezo uliyopewa.

Tunaposoma 1Yohana 3:4 tunapata ufahamu ya kuwa dhambi ni uasi. Kwa hiyo, kutokutenda vyema au kutokutoa sadaka kwa Imani, au kutokufuata maelekezo ya Mungu katika utoaji…

…Kunatengeneza mazingira ya uasi au mazingira yanayovuruga utii na uhusiano wako na Mungu!