Kitabu Kipya cha “MBINU ZA KUMUOMBEA MZALIWA WA KWANZA KAMA LANGO..ili familia yenu ifanikiwe” Hiki ni kitabu cha mwendelezo wa pili katika mafundisho niliyokuwa nayo kuhusu mzaliwa wa kwanza kama Lango, nilichokitoa kwa mara ya kwanza semina ya  mwanza siku ya tano tarehe 25 Julai 2013. Hiki ni kitabu cha pili kukitoa kwa Mwaka huu, Baada ya kile cha “UJUE ULIMWENGU WA ROHO” Nilichokitoa mwezi machi mwaka huu 2013. Katika kitabu hiki utajifunza mambo mengi kuhusu kumwombea mzaliwa wa kwanza yameainishwa katika Sura kama ifuatavyo: -

      1. Unaombaje mauti Inapomwandama Mzaliwa Wako wa Kwanza?....

      2. Tathmini Jinsi Mzaliwa wa Kwanza Anavyohusika Kujenga au Kubomoa Maisha Yako….

      3. Gharama za Kutokuijua kanuni ya mzaliwa wa Kwanza Kama Lango….

      4. Kumwombea Mzaliwa wa Kwanzani Kutii Agizo la Mungu….

      5. Sababu za Msingi Kwa nini ni Muhimu Mzaliwa wa Kwanza Aombewe Zaidi Kuliko Watoto Wengine….

      6. Nani Anastahili Kumwombea Mzaliwa wa Kwanza?....

      7. Namna ya Kuongeza Imani ili Maombi Yako Juu ya Mzaliwa wa Kwanza Yajibiwe…..

      8. Ajenda Muhimu za Kumuombea Mzaliwa wa Kwanza Kama Lango….

      9. Maelekezo ya ziada juu ya Maombi ya kumkomboa Mzaliwa wa Kwanza Asiye na Maisha Mazuri….

    10. Unaombaje ukitaka kumweka wakfu mzaliwa wa Kwanza ilia pate Kulitumikia Kusudi la Mungu?....

    11. Umuhimu wa Kumlinda Mzaliwa wa Kwanza kwa njia ya Maombi…

    12. Maombi kwa Ajili ya Mzaliwa wa Kwanza Yanayounganishwa na Sadaka….

    13. Maombi ya Kufuta Madhara ya Laana za Maneno Yaliyosemwa Juu ya Mzaliwa wa Kwanza….

    14. Muhtasari wa hatua Muhimu Katika Kumwombea Mzaliwa wa Kwanza….